Jumanne, 2 Agosti 2016

KAMPUNI ya Advanced Security Limited imeingia  makubaliano na bingwa wa dunia wa mchezo wa Kareti,  Profesa Maurizio Martina wa Italia kwa ajili ya kutengeneza filamu mbalimbali pamoja na ile inayopinga mauaji ya walemavu wa ngozi, albino na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.
Makubaliano hayo yalifanyika jana kwenye hotel ya JB Delmonte na filamu hiyo itaanza kurekodiwa ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa na kukamilika kwa miezi mitatu.Mwenyekiti wa Kampuni ya Advanced Security Limited, Juma Ndambile alisema kuwa  sababu kubwa ya kuingia katika masuala ya filamu ni moja ya shughuli zake katika kujihusisha na masuala ya jamii.Ndambile alisema kuwa kampuni yao ni Limited na kutokana na hilo inaweza kufanya shughuli nyingine mbalimbali tofauti na huduma ya ulinzi na usalama.Alisema kuwa katika filamu hiyo, atawashirikisha waigizaji mbali mbali wa hapa nyumbani na wapo mbioni kukamilisha taratibu zote kwa mujibu wa sheria ya kurekodi filamu hapa nchini.Kwa mujibu wa Ndambile, Profesa  Maurizio  ambaye ameigiza filamu nyingi katika nchi za mbali mbali pamoja na Uingereza na Marekani mbali ya Italia atashirikiana na mke wake, Angel Howel na mwanaye, Dumiano ambaye amewahi kuigiza na mcheza filamu maarufu duniani.Profesa Maurizio alisema kuwa pia atafundisha wanawake jinsi ya kujilinda kwa kutumia mchezo wa karate ili kuondoa unyanyasaji wa wanawake nchini.Amesema kuwa amefanya kazi  hiyo nchi mbali mbali ikiwa pamoja na DR Congo na Afrika Kusini.“Lengo la filamu yangu ni kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na mila potofu za kuwaangamiza albino na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake,” alisema Profesa Maurizio ambaye pia ni Rais wa Dunia wa Shirikisho la Mchezo wa Kareti.


 Mwalimu wa Karate wa kimataifa Sensei Rumadha 
 Magwiji wa karate duniani wakiwa katika picha ya pamoja katika kongamano la Karate European Jundokan Gasshuku.
..............................................................................................
Sensei Rumadha Fundi mwalimu wa karate mtanzania anatambuliwa na baraza la OKINAWA BODOKAN & KARATE FEDERATION" lenya makao Okinawa,Japan,juzi katika alikuwa ni mwakilishi pekee kutoka Afrika katika kongamano la walimu magwiji wa karate lilifanyika Lisabon,Ureno.
 Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu ni chimbuko la  dojo iliyo jengwa na Master Eiichi Miyazato miaka 63 iliyo pita huko mjini Naha, Okinawa baada ya  kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu , Master Chijun  Miyagi , ambayo hivi sasa  inaendeshwa na mtoto wake Yoshihiro Kancho Miyazato.
 

Sensei Rumadha Fundi, amepokea na kukubali mwaliko kama mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" Tanzania ikiwa natumaini la usajiri wa chama hicho hapa Tanzania ambao kwa sasa bado unalegalega.

Sensei Rumadha yupo nchi Ureno hivi sasa akishiriki katika kongamano la Karate " European Jundokan  Gasshuku 2016".

Na wakati huohuo, kitengo kinachisimamia ubora na uthabiti wa  sanaa asili ya mitindo ya  karate toka Okinawa kiitwacho " OKINAWA BODOKAN & KARATE FEDERATION" imefanya mabadiliko hivi karibuni yatakayo tofautisha  karate asilia na ile ya  kimichezo itayo kuwa katika michezo ya  Olympics.
 

Kutokana na mabadiliko ya  kimbinu na ufasaha yanayo onekana katika michezo, shirikisho hilo limeamua kutofautisha kabisa jinsi karate asilia izidi kuimarika na kutochujwa na kuwa sanaa nyepesi.
  

Pia, kuhakikisha kwa kiundani zaidi kwamba  mbinu halisi,  zinazingatiwa na ma- Sensei wote wa mitindo ya  karate toka visiwani Okinawa duniania kote.
 

 Hivyo ime teuwa timu ya Karate ya Okinawa ( Masters) toka mitindo mbalimbali inayo tambulika na " BUDOKAN" kusambaza uadilifu wa mitindo hiyo kama jinsi ilivyokuwa  inafundisha na waasisi wake asilia.
  

Semina hii inayoendelea nchini Ureno inawawezesha walimu ( Sensei) kuwa na mabadiliko au kuendana sambamba na jinsi sanaa inavyo jadiliwa katika chimbuko lake chini ya shirikisho hilo huko Okinawa,Japan.
  

Tunatumaini kwamba chama cha "JUNDOKAN SO HONBU" kitapata usajili wake nchini Tanzania pasipo fika mwaka 2018, chini ya Sensei Rumadha Fundi mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" Afrika mashariki na Kati. Endapo usajili utaleta kulegalega na kuvuta muda zaidi, basi chama hicho hakitakuwa na budi, bali kitajisajili visiwa vya Zanzibar kwanza. Alimalizia hivyo; sensei Rumadha

js

js

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget